Mvukizo
Mabadiliko ya hali kutoka kimiminika kwenda mvuke, kwa joto lililo chini ya kiwango cha kuchemka. Pamoja na ufupishaji (condensation), ni mojawapo ya taratibu kuu za thermodynamiki zinazotokea katika angahewa, zikihusisha kiasi kikubwa cha joto. Kwa kila gramu ya maji ya kimiminika inayovukiza, karibu kalori 600 hufyonzwa kutoka hewani. Hii ndiyo nishati ya joto inayohitajika kwa gramu hiyo ya maji kugeuka kuwa mvuke.
Istilahilahi zinazohusiana: joto fiche
Pia inajulikana kama: Uvukizi