Iridesensi
Jambo la kuona linaloundwa na mkusanyiko wa rangi zinazojitokeza katika mawingu ya viwango vya juu na vya kati yaliyoko umbali mfupi wa pembe (angular) kutoka jua. Hutokana, mara nyingi, na mtawanyiko wa mwanga (diffraction). Laweza kujitokeza na rangi zikiwa zimechanganyikana au zikiunda mikanda inayokaribia kufanana na mipaka ya wingu, ambapo rangi za kijani hafifu (pastel) na waridi hutawala. Ukaribu wa duara la jua (chanzo cha mwanga) na mawingu yenye iridesensi hufanya iwe vigumu kuiona. Kuvaa miwani ya jua ya polarized huwezesha kuiona kwa uwazi.