IPCC
Kifupi cha Jopo la Serikali Mbalimbali kuhusu Mabadiliko ya Tabianchi (Intergovernmental Panel on Climate Change), pia linalojulikana kama Jopo la Kiserikali kuhusu Mabadiliko ya Tabianchi. Ni chombo cha kimataifa chini ya Umoja wa Mataifa, kilichoanzishwa mwaka 1988 na Shirika la Hali ya Hewa Duniani (WMO) na Mpango wa Mazingira wa Umoja wa Mataifa (UNEP). Kazi yake kuu ni utengenezaji wa tathmini za mara kwa mara za hali ya maarifa ya kisayansi, kiufundi, na kijamii-kiuchumi kuhusu mabadiliko ya tabianchi, ikijulisha jamii kuhusu visababishi vyake, athari zake zinazowezekana, na mikakati ya kufuata ili kujirekebisha (adapt) na kupunguza athari zake. Maelfu ya wanasayansi na wataalamu duniani kote, katika taaluma mbalimbali zinazohusiana na mabadiliko ya tabianchi yaliyotajwa, hushiriki katika kutengeneza ripoti za tathmini za IPCC.