Mnururisho wa Jua
Kiasi cha mnururisho wa jua wa moja kwa moja kinachogonga kila kipimo cha eneo katika kiwango fulani. Kwa kawaida hurejelea aidha mnururisho unaofika kileleni mwa angahewa au ule unaofika kwenye uso wa Dunia. Huonyeshwa kwa W/m2 na hutegemea kigezo cha jua (solar constant), msimu wa mwaka, latitudo, na kiwango cha uwazi wa hewa. Neno hili pia laweza kurejelea nguvu au jumla ya kiasi cha mnururisho wa jua (wa moja kwa moja + uliotawanyika) unaogonga kila kipimo cha eneo la mlalo, pamoja na masaa ya jua; ambayo katika Hali ya Anga ni sawa na muda ambao, katika kipindi cha siku, jua huangaza bila kufunikwa na mawingu.
Istilahilahi zinazohusiana: heliografu / kipima muda wa jua