Kituo cha Hali ya Hewa Kinachojiendesha (AWS)

Kikiwa na moduli mbalimbali na kuwa na vitambuzi (sensor) mbalimbali, vituo hivi vinaweza kukusanya data za hali ya hewa, kutengeneza grafu kwa data hizo, kuzihifadhi na kuzisambaza kiotomatiki, kupitia Mfumo wa Mawasiliano ya Kimataifa (Global Telecommunication System) wa Shirika la Hali ya Hewa Duniani, bila kuhitaji watu wanaosimamia kufanya kazi hizo zote. Uingiliaji wa binadamu unahitajika tu kwa kazi za ukarabati na matengenezo, pamoja na kupakua data, endapo AWS haiwezi kuzituma. Mitandao ya AWS huongezea ile ya vituo vya kawaida vya ardhini na hutumika kwa madhumuni ya tabianchi na pia kwa kazi za ufuatiliaji wa hali ya hewa.