mwanga wa zodiaki
Koni ya mwanga mweupe au wa manjano, wenye nguvu ndogo na mwonekano wa maziwa, unaotokea angani usiku kwenye tabaka la ekliptiki. Huonekana hasa katika maeneo ya kitropiki, ikiwa kuna giza la kutosha na hewa ni safi. Chini ya hali hizo, mwanga wa zodiaki huanza kuonekana baada ya jua kuzama - mara tu gizagiza la jioni linapokwisha - na kutoweka mwishoni mwa usiku, kunapoanza kupambazuka. Husababishwa na mtawanyiko unaopitia mwanga wa jua unapopita kati ya chembechembe nyingi za vumbi la anga zilizopo katika nafasi ya sayari kwa sayari.