kuzoea

Marekebisho katika mifumo ya kiikolojia, kijamii, au kiuchumi ambayo lengo lake kuu ni kupunguza hatari zinazohusiana na mabadiliko ya tabianchi, na kutufanya tusiwe rahisi kuathirika nazo. Hatua za kuzoea ni mkusanyiko wa vitendo vya kufanywa kukabiliana na athari za sasa na za baadaye za mabadiliko ya tabianchi. Kutegemea kiwango cha utekelezaji wake, madhara yanayoweza kutokea kutokana na tabianchi yatapunguzwa kwa kiwango kikubwa zaidi au kidogo, hivyo kufikia uwezo mkubwa au mdogo wa kuhimili (resilience).