Uyeyukaji

Mabadiliko ya hali ya dutu, kutoka awamu ngumu kwenda kimiminika. Uyeyukaji wa barafu ni mojawapo ya taratibu za kawaida zaidi katika angahewa. Hutokea katika baadhi ya hydrometeo zinapoanguka (theluji, mvua ya mawe...) na pia ndani ya mawingu au katika milundo ya barafu, inayogusana na hewa, iliyoko juu ya uso wa Dunia (barafu za milimani (glaciers), barafu ya baharini, mabamba ya barafu au theluji...). Kwa kila gramu ya barafu inayoyeyuka, karibu kalori 80 hufyonzwa kutoka hewani. Hii ndiyo inayojulikana kama joto fiche la uyeyukaji (latent heat of fusion).