wavu wa gridi

Kundi la vituo (points) ambavyo mfano wa kihesabu wa utabiri wa hali ya hewa au hali ya anga husambaza na kufafanua kwa kiasi cha nafasi vigezo mbalimbali unavyotumia. Umbali kati ya vituo viwili vya gridi vilivyo karibu huwakilisha uwezo wa mtenganisho wa kinafasi (spatial resolution) wa mfano husika. Kwa sasa, mifano ya mzunguko wa jumla (general circulation models, GCMs) hufikia mtenganisho wa kati ya kilomita 10 na 20. Changamoto katika miaka ijayo - huku uwezo wa kikokotoo wa kompyuta kuu (supercomputers) ukiendelea kuongezeka - ni kuleta mtenganisho wa GCMs hadi kilomita 5.

Pia inajulikana kama: gridi