kinasa ukungu
Kifaa ambacho sehemu yake kuu ni skrini kubwa yenye wavu mwembamba sana uliotengenezwa kwa nyenzo ya sanisi kama vile polipropelini, ambayo ina uwezo wa kunasa matone madogo sana ya ukungu, na kuruhusu kukusanywa na kuhifadhiwa. Skrini hizi zinafanikiwa kutoa maji safi ya kunywa kwa baadhi ya jamii ndogo zinazoishi katika maeneo ya jangwa ambako mvua ni haba sana, kama vile Atacama, nchini Chile.
Pia inajulikana kama: Kikusanya Ukungu, Skrini ya Kukamata Ukungu