Muunganiko wa matone

Katika fizikia ndogo ya mawingu (cloud microphysics), huu ni mchakato ambao kwa njia yake tone (au tone dogo) la maji ya kimiminika huundwa kwa kuungana kwa matone mawili au zaidi, baada ya kugongana yenyewe kwa yenyewe. Kanuni ya mgongano-muunganiko ni mojawapo ya zile zinazosababisha kuundwa kwa matone ya mawingu na matone ya mvua angani.