Barografu
Ni barometa ya aina ya aneroid iliyowekewa kifaa chenye uwezo wa kurekodi shinikizo la hewa kwa mfululizo. Mitikisiko inayopatikana na kifuko cha aneroid - kutokana na mabadiliko ya shinikizo - hupelekwa kwenye kalamu inayogusa karatasi yenye alama za kipimo iliyowekwa juu ya silinda inayozunguka. Ncha ya kalamu yenye wino huchora mchoro (graph) juu ya karatasi hiyo, ikionyesha kwa usahihi mabadiliko ya shinikizo, pamoja na kupanda na kushuka kwake kwa mfululizo. Chombo hicho ni lazima kirekebishwe (calibrated) mara kwa mara (vyema kila baada ya saa 24) kwa kulinganishwa na barometa ya zebaki, kutokana na usahihi mkubwa zaidi wa chombo cha mwisho.
Istilahilahi zinazohusiana: shinikizo la hewa