mzunguko wa hidrolojia
Mzunguko wa asili unaojumuisha taratibu zote zinazohusika katika usafirishaji wa maji yaliyomo Duniani. Uvukizi wa maji kutoka baharini na mvua - kufuatia kuganda kwa mvuke wa maji angani (condensation) - ndizo taratibu kuu za mzunguko wa hidrolojia, unaojulikana pia kama mzunguko wa maji.