Kipindi cha upepo

Katika lugha ya baharini, ni muda ambao upepo uleule huvuma bila kukatika. ("Kupanda kukubwa kunakofuatiwa na kushuka kukubwa [ikimaanisha kipimo cha shinikizo la hewa, barometa], ni ishara ya hakika ya kipindi kirefu zaidi cha upepo kinachokuja," inasema kanuni inayotumiwa na mabaharia).