puto lililofungwa

Puto la hali ya hewa lililofungwa ardhini kwa kamba, jambo linaloruhusu vipimo kufanywa katika kimo kinachotakiwa. Hutumika hasa katika kampeni za kisayansi, kwa madhumuni maalum; pale panapokuwepo hitaji la kujua jinsi kigezo fulani cha hali ya hewa kinavyofanya kazi katika kiwango fulani cha angahewa.